Monday, May 22, 2006

Ukweli kuhusu Wanyama

WANYAMA
Duniani kuna aina nyingi sana ya viumbe kama vile ndege, wanyama, samaki, wadudu na wengineo, na viumbe wote hao wanatabia , maumbile,mahitaji mapendo na mifumo mbalimbali ya kuendesha maisha mbali ya msaada wa binadamu kwa asili ya maisha ya viumbe wa duniani. Pia kuna wanyama ambao wana akali ya kutambua na kufanya vitu mbalimbali karibia kabisa na binadamu, na sifa kubwa zaidi kwa viumbe wengi ni kuwa wanalea na kuwatunza watoto wao.

Haki za Wanyama
Nini maana ya haki za wanyama?

Haki za wanyama maana yake wanyama wana aina Fulani ya kufikirika, kuthaminika—kufikirika, kuthaminika kutokana na nini bora kwa mapenzi, mahitaji, na maamuzi yao kutokujali kama hawasikii, wanatumiwa na binadamu, au wanakaribia kutoweka na kutokajali kama wanatunzwa na binadamu {kama ilivyo kwa binadamu aliyepungukiwa na akili anaayo haki hata kama watu wote hawampendi} ina maana kutambua kuwa wanyama siyo wetu kwa ajili ya chakula, kuvaa, kiburudisho, au majaribio ya kisayansi.

Ni Haki Zipi za Wanyama ?
Wanyama wanahaki ya kuthamiwa kwa maamuzi yao wenyewe kwa mfano, mbwa ana maamuzi ya kutokuwa na maumivu anayoyapata pasipo kuwa na sababu yeyote ile, maana, kwa hiyo tunalazimika kuchukua maamuzi yao katika kuwathamini na kuwajali mbwa kuwa na haki ya kutokuwa na maumivu yasiyo ya lazima anayoyapata.

Hata hivyo wanyama kawida hawana haki zinazofanana na binadamu, kwa sababu maamuzi na mahitaji yao kawida hayafanani na yetu, na baadhi ya haki zinaweza kuwa kinyume na maisha ya wanyama, kwa mfano, mbwa hana maamuzi, hafahamu haki ya kupiga kura na kwa hiyo hana haki ya kupiga kura, tangu hapo haki hiyo itakuwa haina maana kwa mbwa na kama ilivyo kwa mtoto.

Umesimama Wapi?
Kuna baadhi ya bianadamu ambao kwa huruma na upendo wanaweza kusimama na kumtoa jongoo barabarani na kumpeleka sehemu salama. Kujali matatizo na kuwajibika ni maadili yanayopanuka na tunalazimika kuishi kila siku kwa kuhukumu na kuhukumu kuamua kila kitu kinachotokea kwa ubaya na uzuri kama tunavyoweza.

Hatuwezi kuzuia mateso yote, lakini haina maana kuwa hatuwezi kuzuia mateso yeyote katika maisha ya sasa ya duniani yenye muenekano wa mapungufu ya uchaguzi, kawaida huwa kuna huruma na ubabe, njia ambazo wengi wetu tunazotumia katika kula, kuvaa, kuburudika, na kujifunza sisi wenyewe kuliko kuua wanyama.Vipi Miti na Mimea?
Hakuna njia inayoonyesha tuamini kuwa miti na mimea inahisi maumivu, kwani haina mishipa ya fahamu “ubongo”na mwisho wa mishipa ya fahamu. Sababu pekee inayoonyesha kuwa wanyama wanahisi maumivu ni jinsi watakavyo jihami.
iwapo utashika kitu ambacho kitakuumiza au kujeruhi, maumivu yatakufundisha kutokugusa na kukiacha pekee siku nyingine. Tangu hapo miti na mimea haiwezi kutembea kuepuka maumivu na hivyo haitaji kijifunza kuepuka baadhi ya vitu.

Imani Katika Haki Za Wanyama
Ni vizuri kuamini katika haki za wanyama kwani kila mtu anawajibika katika maamuzi yake, lakini “uhuru wa kufikiri” kawaida huwa hauwendani na “uhuru wa kutenda”. Upo huru kuamini chochote unachotaka ingawaje huwaumizi wengine, unaweza kuamini kuwa wanyama ni lazima wauwawe, kwamba watu weusi ni lazima wawe watumwa, au mwanamke ni lazima apigwe, lakini hufanyi imani yako uiweke kwenye majaribio- yaani kwa kutenda.

Wanyama hawazielewi haki zao, mara nyingi hawaheshimu haki zetu, je ni kwanini tunatoa mawazo yetu ya kiroho juu yao?
Kwa sababu wanyama kushindwa kufahamu na kuingia katika miongozo yetu ni sawasawa na mtoto mdogo au kichaa kushindwa kufana hivyo. Wanyama hawako, hawana, au hawajawezeshwa kuchagua kubadilishwa tabia zao, lakini binadamu anayo akili ya kuchagua kati ya tabia zinazowaumiza wengine na kutokuwaumiza wengine.

Ni vigumu kuepuka kutesa wanyama na mara nyingi hufanyika bila kufahamu?
Ni kweli ni vigumu kuishi maisha yako bila ya kuleta majeruhi kwa viumbe wote, kwa bahati mbaya tumeshakanyaga siafu na viumbe wengine, lakini haina maana kuwa tumedhamilia kuwakanyaga siafu hao. Lakini kwa sababu unaweza kusababisha ajali kwa kumgonga mtu na gari haina maana kumfanya bianadamu awe ni kwa ajili ya kugongwa na gari.

Vipi kuhusu mila, tamaduni, na kazi zinazotegemea kutumia wanyama?
Uanzishaji wa magaari, uzuiaji wa biashara ya utumwa, na mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia kulilazimisha kutokea na mifumo mingine ya kufanya kazi na kuiendeleza. Hii ilikuwa ni chachu katika maendeleo jamii za binadamu—siyo sababu ya kuvuruga maendeleo.

Wanyama wengi wanaotumika kwa chakula, kazi, manyoya, ngozi na majaribio ya kisayansi wamezaliwa kwa ajili hiyo?
Kwa kuzaliwa kwa shughuli hiyo hakuwewzi kubadilisha uwezo wa kibaolojia wa mnyama kusikia maumivu na huzuni.

Mungu ameweka wanyama hapa duniani kwa ajili ya kuwatawala, vitabu vya dini vimetupa utawala juu wanyama?
Kutawala siyo sawasawa na kutawala kwa mabavu na utesaji, mfano, Rais wa Tanzania anatawala au anawaongoza watanzania, lakini haina maana kuwa anaweza kuwala au kuwatesa watanzania. Iwapo tunatawala wanyama, ukweli kabisa ni kuwalinda, siyo kuwatumia kwa mahitaji yetu. Hakuna chochote kwenye vitabu vya dini kinachoweza kuelezea maisha yetu ya sasa na mipangilio ambayo inaharibu mazingira, kuharibu na kutokomeza vizazi vya wanyama wa porini na vifo vya wanyama kila mwaka.

Je ni kweli wanyama wanaofungiwa muda wowote hawateseki kwa sababu hawajui kitu chochote kile?
Kuzuiwa kufanya karibia vitu vyote vya asili kitabia kunasababisha maumivu au usumbufu wa hali ya juu hata kama mnyama amefungiwa tangu azaliwe anahitaji kutembea, kugusana pamoja kunyoosha miguu yao au mabawa yao na mazoezi. Wanyama wanaochungwa, na wanyama wanaotembea kikundi huwa wanapata kuchanganyikiwa wakati watakapoishi kwa kutenganishwa au watakapowekwa kwenye makundi makubwa ambapo wanashindwa kutambuana.

Iwapo utumiaji wa wanyama ungekuwa ni makosa ingekuwa ni uvunjaji wa sheria?
Utawala wa sheria siyo kinga ya imani ya kiroho, nania ametenda kosa na nani hakutenda kosa kisheria huamuliwa na maoni na mapendekezo ya wanasheria wa sasa, sheria zinabadilika kama mapendekezo ya jamii au mabadiliko katika siasa yatabadilika, lakini maadili hayabadilki. Angalia baadhi ya vitu ambavyo kwa wakati Fulani ilikuwa ni sheria dunia ajira ya mtoto, utumwa wa binadamu, na ukandamizwaji wa wanawake.

Wanyama hawana akili au wameendelea kama binadamu?
Kuwa na uwezo na akili nyingi hakumaanishi binadamu mmoja kumnyanysa mwingine kwa malengo yake, kwanini binadamu mwenye akili anyanyase wasio kuwa bindamu. Kuna wanyama ambao wana akili, wabunifu, wanaojali, wanaowasiliana na wenye uwezo wa kutumia lugha kuliko baadhi ya bianadamu , kama ilivyo kwa sokwe mtu akilinganishwa na mtoto mchanga au kichaa wa hali ya juu sana, je itakuwa wanyama wenye akili kuwa na haki na binadamu wenyekili kidogo kunyimwa haki?

Mwanaharakati wa haki za wanyama Tanzania
animalactivisttz@yahoo.com

Saturday, May 20, 2006

Haki za wanyama Tanzania

USAFIRISHAJI WA NG’OMBE

Tanzania imejaliwa kuwa na viumbe hai wengi, wakiwemo Binadamu na N’gombe.
Ng’ombe ni mifugo inayofugwa katika kila sehemu ya nchi yetu, kwani ni pato lianlotegemewa kuendeshea maisha ya watu wengi vijijini na mijini.

Kutokana na Ng’ombe kuwa ni pato linalotegemewa na wengi, hivvo kumekuwa na biashara kubwa ya Ng’ombe katika kila pembe ya nchi yetu hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na sehemu nyingine.

Jiji la Dar es salaam linakadiriwa kupokea Ng’ombe zaidi ya 100 kwa siku kutoka katika mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya na sehemu nyingine. Ng’ombe hao husafirishwa kwa njia ya Barabara na Reli, yaani, kwa kutumia magari na mabehewa.

Safari ya kusafirisha Ng’ombe kuelekea Dar es Salaam inachukua siku kadhaa kutegemeana na umbali wanakotoka. Kwa mfano, Ng’ombe kutoka Shinyanga kwa njia ya Treni inachukua kati ya siku 5-7 mpaka kufika kwenye mnada wa pugu.

Kawaida kisheria katika kusafirisha wanyama kwa njia Treni kuna mabehewa maalumu ya kubebea wanyama kama Ng’ombe ambayo yanakuwa na paa la kuzuia mvua na jua, na madirisha makubwa kwa ajili ya kupitisha hewa, pia Ng’ombe wanatakiwa kuhudumiwa chakula na maji katika safari yao.

“Lakini ikumbukwe kuwa wanyama wanahisi maumivu kama ilivyo kwa Binadamu”.

Kitendo cha kusafirisha Ng’ombe kwenye mabehewa yasiyokuwa na paa la kuzuia mvua na jua, kujaza Ng’ombe kupita kiasi na kuwabana kama mizigo, kuwanyima chakula na maji kwa siku kadhaa, kuwachapa kwa kutumia fimbo au kitu chochote kile na kuwafinya mikia.
Ni ukatili wa hali ya juu kwa Taifa lianalojigamba kuwa na amani na lenye kufuata mfumo wa demeokarsia.

Angalia tena manyanyaso mengine ya Ng’ombe kwa njia ya Barabara. Ng’ombe wanasafirishwa kutoka mikoani kwa kutumia magari ambayo kisheria hayakidhi matakawa ya kusafirisha Ng’ombe.
Wafanyabiashara wanatumia magari ya mizigo ambayo hayana paa la kuzuia mvua na jua na ili waendelee kupata faida kubwa, basi Ng’ombe watajazwa na kubananishwa kama mizigo kiasi kwamba wanakosa hata nafasi ya kugeuka au kukaa chini, kibaya zaidi ni pale wasindikizaji wanapokuwa wanawapiga sana Ng’ombe kwa kutumia fimbo, na pia ikitokea Ng’ombe atakaa chini basi huo unaweza ukawa mwisho wa maisha yake ndani ya safari kwa kukanyagwa na wenzie, hii yote inatokana na kubanana kama mizigo.

Embu angalia pale kwenye mnada wa mifugo wa Pugu unaosimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo, pale kuna Afisa Mifugo, Askari Polisi na pembeni kuna Kituo kidogocha Polisi, lakini hata siku moja sijasikia mtu kashitakiwa kwa kumnyanyasa Ng’ombe, je Afisa Mifugo na Askari Polisi hawafahamu kuwa kuna sheria zinazowalinda wanyama kutokupata manyanayaso yanayotendeka pale? kwani utakuta Ng’ombe wanapigwa sana hasa wakati wa kupakia na kuwashusha.
Kibaya zaidi Ng’ombe watajazwa na kulazimishwa kuingia kwenye magari hata kama nafasi hakuna, na pia ukibahatika kuwaona Ng’ombe wanaoshushwa kwenye magari au mabehewa utawaonea huruma sana kwani utawaona wengi matumbo yao yameingia ndani,yaani wananjaa ya muda mrefu, wamechoka sana na wengine wamekonda.

Na pia huwa kunakuwa na watoto wa Ng’ombe {ndama} ambao kisheria hawaruhusiwi kupelekwa pale, na ndio maana Ng’ombe wote wakifika pale ni lazima wapelekwe wakanywe maji na kula majani, na kupigwa mnada siku inayofuata.

Je serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mfugo inafanya nini katika kilinda na kutetea maslahi ya wanyama hao, au shughuli yao kubwa ni kukusanya mapato tu?
Taifa jema litaonekana jema iwapo litajali Binadamu na viumbe hai wote wakiwemo Ng’ombe.

Ukweli ni kwamba iwapo walaji wa nyama ya Ng’ombe wangeona na kutambua ni jinsi gani Ng’ombe wanavyotendewa ukatili kabla ya kuchinjwa wangeacha mara moja kula, kwani inafahamika kuwa Binadamu ameumbwa kuwa na huruma

Lengo langu siyo kuzuia biashara ya Ng’ombe ila ni kutoa dukuku langu la muda mrefu ambapo ninasosoneneka sana nikiona Ng’ombe wakiteseka ndani ya nchi yetu bila ya kuona waliyopewa jukumu la kusimamia mifugo hawashituki wala kuchukua hatua zozote kwa wanaovunja sheria za haki za wanyama nchini Tanzania

Mwisho naomba wizara ya maendeleo ya mifugo ambayo ipo chini Serikali ya Muheshimiwa Jakaya M, Kikwete yenye kauli mbiu ya Kasi Mpya, Ari Mpya, na Nguvu Mpya. Watumie kauli mbiu hii kuleta maslahi bora ya haki za wanyama kufuata Kanuni, Taratibu na Sheria za Nchi za usafirishaji wa Wanyama.

Mtetezi wa haki za wanyama
Animalactivisttz@yahoo.com
0746 027419